HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 27, 2013

Makamu wa Rais,Dkt. Bilal afunga Mafunzo ya Uofisa na Ukaguzi wa Jeshi la Polisi,Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini jijini Dar leo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal akikagua Gwaride Maalum lililoandaliwa na Wahitimu wa kozi ya Uofisa na Ukaguzi wa Jeshi la Polisi leo katika Chuo cha Taaluma ya Polisi, Kurasini, Jijini Dar Es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal akimvisha Cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Mhitimu wa Kozi ya Ukaguzi wa Polisi INSP. Leah Cheyeki kwa niaba ya Wahitimu wenzake kutokana na kufanya vizuri katika Mafunzo hayo. Sherehe za kuhitimisha Mafunzo hayo zimefanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi leo Kurasini, Jijini Dar es Salaam.
Wahitimu wa kozi ya Uofisa na Ukaguzi wa Polisi wakipita mbele ya Mgeni Rasmi kwa mwendo wa haraka Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayupo pichani. Sherehe za kuhitimisha Mafunzo hayo zimefanyika leo katika Chuo cha Taaluma ya Polisi, Kurasini, Jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Judo kikionesha Onesho Maalum la namna ya kupambana na Mhalifu ambaye hataki kutii amri halali ya Polisi. Sherehe za kufunga Mafunzo ya Kozi ya Uofisa na Ukaguzi wa Polisi zimefanyika Chuo cha Taaluma ya Polisi, Kurasini, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dkt. Emmanuel John Nchimbi(wa pili kutoka kushoto mwenye suit nyeusi)akiwa na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama ambao wamehudhuria Sherehe hizo za ufungaji Mafunzo ya Kozi ya Uofisa na Ukaguzi wa Polisi(katikati) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja.
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria Sherehe za Ufungaji Mafunzo ya Kozi ya Uofisa na Ukaguzi wa Polisi katika Chuo cha Taaluma ya Polisi, Kurasini Jijini Dar es Salaam(Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad