HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 27, 2013

OCD MAKETE AWAASA WAHUDUMU WA NYUMBA ZA KULALA WAGENI KUWAANDIKISHA WATEJA WAO

Na Edwin Moshi, Njombe.

Jeshi la polisi wilayani Makete mkoani Njombe limewataka wamiliki wa nyumba za kulala wageni wilayani hapo kuhakikisha wanaandikisha taarifa za wageni wanaofika kulala kwenye nyumba hizo, kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kuwaweka salama pindi kunapotokea tatizo.

Hayo yamesemwa na mkuu wa polisi wilaya ya Makete SP Peter Kaiza wakati akizungumza katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo kuhusiana na tabia ya baadhi ya wahudumu wa nyumba za kulala wageni kudharau kuandikisha taarifa zinazowahusu wageni kwa kinachodhaniwa kuwa ni kuwaibia wamiliki kwani suala hilo ni hatari kwao na kwa jeshi la polisi pia.

“Akuja mgeni kulala kwenye nyumba unayofanyia kazi, wewe hujampa daftari akandika jina na taarifa zingine, usiku linatokea la kutokea mtu ananyooka(anakufa) sasa utajibu nini kwa bosi wakao na kuja kutoa taarifa polisi utaanza anza je” alisema Kaiza.

Katika hatua nyingine kaiza amezungumzia dhana iliyojengeka kwa wahudumu hao kuwa wateja wengi huandika taarifa za uongo hivyo kuona hakuna haja ya kuandika taarifa zao akisema si kweli kuwa kila taarifa itakuwa ya uongo na kusisitiza kuwa wawaandikishe kwa kuwa zitasaidia pindi likitokea tatizo.

Kwa upande wake afisa biashara wilaya ya Makete Bw. Adonia Mahenge(PICHANI) amesema ni vyema wahudumu wa afya wakatambua umuhimu wa kutunza taarifa hizo kwani ni suala la kisheria ambalo linatakiwa kufuatwa na kila mhudumu wa nyumba ya kulala wageni.

Amesema katika kusisitiza hilo watafanya ukaguzi muda wowote kuona kama hatua hizo zinafuatw na ambaye atakuwa amekiuka utaratibu atachukuliwa hatua kali za kisheria, waweke mabango yanayoonesha utaratibu na kanuni na masharti ya kulala kwenye nyumba ya wageni, kuboresha nyumba hizo ikiwemo usafi na ubora wa huduma.

Amesema maazimio hayo yanatakiwa kutumika ndani ya wilaya nzima ya Makete ikiwemo Makete mjini, Ikonda, Bulongwa, Matamba na maeneo mengine ambayo nyumba hizo zipo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad