HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 27, 2013

WASHIRIKI WA REDD’S MISS KANDA YA MASHARIKI 2013 WATEMBELEA MAENEO MBALIMBALI MJINI MOROGORO

Na John Nditi ,Morogoro.

WAREMBO wanaoshiriki kinyang’anyiro cha Redd’s Miss Kanda ya Mashariki 2013 , inayoundwa na mikoa ya Pwani, Lindi, Mtwara na Morogoro, Juni 27, mwaka huu, wamefanya ziara ya kutembelea Kituo cha Amani , banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na la TACAIDS mkoa wa Morogoro.

Kituo cha Amani kilichopo katika Kata ya Chamwino, Manispaa ya Morogoro ambacho kinamilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro ni cha kuwalea Watoto wenye Ulemavu wa viungo na mtindio wa ubongo.

Washiriki hao waliongozwa na Mratibu wa Shindano hilo, Alex Nikitas pamoja na mlezi ‘ matron’ wao Kudra Lupatu, ambaapo katika Kituo hicho walipokelewa na Mkurugenzi wake Padre Beatus Sewando na wasaidizi wake.

Walielezwa historia fupi na Mkurugenzi huyo , kuwa kituo kinawapokea watoto wenye ulemavu wa aina hiyo kutoka ndani na nje ya mkoa wa Morogoro , ambapo pia walitembezwa katika vyumba vya kulala na wao pia kupata fursa ya kuuliza mswali kabla hatua ya kutoa zawadi zao kwa uongozi wa Kituo hicho.

Washiriki hao pia walitembelea baadhi ya mabanda ya maonesho kwenye uwanja wa Jamhuri wa Mjini Morogoro yanakofanyika maadhimisho ya wiki ya Serikali za Mitaa Kitaifa.

Mabanda waliyotembelea ni la Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi ( TACAIDS) mkoa wa Morogoro na baadhi yao waliamua kupima damu zao.

Washiriki hao pia walitembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na kila mmoja alipima uzito pamoja na urefu kwa lengo la kubaini uwiano wa miili yao.

Kinyang’anyiro hicho cha shindano hilo kimepangwa kufanyika Juni 29, mwaka huu kwenye ukumbi wa Hoteli ya Nashera ya mjini hapa.

Warembo 14 wanawania taji hilo ambapo shindano hilo limedhaminiwa na Redd’s Original , Michuzi Blog, Dodoma Wine, CXC Africa, Nyumbani Park, Usambara Safari Lodge,Chilakale Resorts, Big Solution , Nashera Hotel na Mikocheni Resort Centre.

Mratibu wa Shindano hilo , Nikitas, aliwataja washiriki hao ni Muzne Abduly (19), Ummy Mohamed (21), Sabra Islam (19) na Diana Laizer (21) wote kutoka Mkoa wa Morogoro.

Wengine ni Ivony Stephen (22),Pulkeriah Ndovi na (21)Zulfa Semboja (19) kutoka mkoa wa Mtwara na kutoka mkoa wa Lindi ni Janeth Awet (19), Zainabu Shaaban (23 na Sophia Maganga (21).

Mkoa wa Pwani, washiriki wake katika kinyang’anyiro hicho ni, Elizabeth Perty (22),Suleiyah Abdi (22),Easther Albert (20) pamoja na Lilian Joseph (21).
Warembo wakabidhi msaada wa mafuta ya kula.
Baadhi ya washiriki wa Redd's Miss Kanda ya Mashariki ( kushoto) wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kituo cha Amani cha watoto wenye Ulamavu wa Viongo na Mtindio wa Ubongo, Padre Beatus Sewando.
Picha ya pamoja eneo la Kituo cha Amani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad