HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 3, 2013

MEYA WA MANISPAA YA ILALA ATEMBELEA MAONYESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA - SABASABA LEO

IMG_8797
Mstahiki Meya Jerry Silaa akisalimiana Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal walipokutana kwenye Banda la Mfuko wa Fursa sawa kwa wote (EOTF) kwenye viwanja vya maonyesho ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar.
IMG_8830
Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Mama Anna Mkapa akiagana na Mstahiki Meya Jerry Silaa mara baada ya kutembelea Banda la (EOTF) linalotoa fursa kwa wajasiriamali nchini Tanzania kuonyesha bidhaa zao katika maonyesho hayo kila mwaka.
IMG_8735
Mkurugenzi Mtendaji wa Home Shopping Centre (HSC) Fahad Said Mohamed (kushoto) akimkaribisha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa kwenye Banda la HSC kwenye maonyesho ya 37 kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
IMG_8808
Mtsahiki Meya Jerry Silaa akipewa maelezo ya jinsi Mfuko wa Fursa sawa kwa wote unavyopambana na kutokomeza Ugonjwa wa Saratani ya Matiti kwa wakina mama nchini. Kushoto ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Mama Anna Mkapa.
IMG_8558
Mstahiki Meya Jerry Silaa akipata maelezo jinsi ya kutumia Kizimamoto Fanisi cha kurusha (Fire Extinguisher) ambacho ni rahisi kutumia na hakihitaji matengenezo na hudumu kwa miaka mitano pia Kifaa hicho ni rafiki wa mazingira na mvumbuzi bora kwa uokoaji wa dharura wakati alipotembelea Banda la GreenBat Fire Solutions katika maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea.
IMG_8542
Mstahiki Meya Jerry Silaa akisaini kitabu cha wageni katika banda la Arusha International Conference Centre (AICC) wanaoshughulika kutoa huduma za kumbi za Kimataifa za mikutano na Utalii jijini Arusha.
IMG_8531
Mstahiki Meya Jerry Silaa akingalia jinsi mtoto Range Jackson ( wa pili kushoto) mwenye ulemavu wa Ubongo akionyesha ramani ya Tanzania na Sehemu ya mipaka yake iliyotumika kumfundishia kujua kusoma na kuandika na ufundi stadi kupitia kituo cha VETA. Kulia ni Mkufunzi wa kuchomea (Welding Instructor) na Mwalimu wa watu wenye mahitaji maalum Bw. Kintu Kilanga na Wa tatu kulia ni Baba mzazi wa kijana huyo Bw.Jackson Range.(Picha na Zainul Mzige).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad