HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 3, 2013

SERIKALI YAKABIDHIWA RASMI UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR LEO

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangaraka (kulia) akipokea Ufunguo wa mfano kutoka kwa Balazo wa China hapa nchini Balozi Lu Youging kuashiria kukabidhiwa rasmi kwa Uwanja wa Taifa.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara (Kulia) akishuhudia Balazo wa China hapa nchini Balozi Lu Youging akiweka sahihi katika hati ya makabidhiano ya Uwanja wa Taifa.Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga(Kushoto) akitia sahihi katika hati ya makabidhiano ya uwanja wa Taifa,kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi Habib Mkwizu.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara (Katikati) akishuhudia Balazo wa China hapa nchini Balozi Lu Youging akibadilishana hati ya makabidhiano ya Uwanja wa Taifa na Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga (Kulia).
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Utumishi Habib Mkwizu (Kushoto) akifafanua jambo kwa baadhi ya viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo mara baada ya sherehe ya makabidhiano ya Uwanja kukamalizika.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Assah Mwambene (Kulia) akizungumza akibadilishana mawazo na Katibu Mtendaji wa TFF Angetile Oseah walipokutana katika sherehe za makabidhiano ya Uwanja wa Taifa jana jijini Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA FRANK SHIJA - MAELEZO.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad